2 Agosti 2012 - 19:30

Jeshi la Syria limeeleza kuwa Mji wa Rif umeshasafishwa na hakuna tena magaidi.

Ripoti ya Shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Jeshi la Syria limeeleza kuwa: Mji Mkuu wa Syria sasa upo katika amani kwani sasa Jeshi la Syria limefaanikiwa kuondowa magaidi katika Mji wa Rif ulokuwa pembezoni mwa Mji Mkuu wa Syria

Aidha Jeshi la Syria katika Mji wa Kufr Halab limeshika magaidi kadhaa na baadhi yao kuuawa katika mapigano hayo.

Mji Mkuu wa Syria katika wiki ilopita ilishuhudia mapigano ya hapa na pale kwa kuvamiwa na waasi wa Nchi hiyo.

Hadi sasa Mkoa wa Halab bado kunamapigano baina ya Jeshi la Nchi na waasi, Jeshi la Syria limearifu kuwa karibuni Mkoa wa Halab pia utasafishwa kama Mikoa mingine.

Syria myezi 17 ilopita imeshuhudia mapigano na kuingilia Nchi za kimagharibi katika masuala ya Nchi hiyo.